Blog / Job Board Guides / Nafasi 678 mpya za ajira serikalini MDAs na LGAs mwezi Septemba 2026

Nafasi 678 mpya za ajira serikalini MDAs na LGAs mwezi Septemba 2026

By System Administrator • Published 05 Sep 2026 • 👁 74 Views
Cover

1.0 DAKTARI DARAJA LA II (MEDICAL OFFICER GRADE II) - Nafasi 115
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa
mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina mama na
upasuaji wa kawaida na wa dharura.
ii. Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika
Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
iii. Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
iv. Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
v. Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi za Kufundisha
wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi.
vii. Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake.
viii. Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
ix. Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
x. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
xi. Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality
improvement).

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika
(Medical Council of Tanganyika).
1.3 NGAZI YA MSHAHARA
 TGHS E


2.0 AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT NURSING OFFICER
GRADE II) - Nafasi 128
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutoa huduma za uuguzi.
ii. Kukusanya takwimu muhimu za afya.
iii. Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
iv. Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo ya kiafya.
v. Kutoa huduma za kinga na uzazi.
vi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi, ya muda usiopungua miaka miwili
kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na
Wakunga Tanzania
2.3 NGAZI YA MSHAHARA
 TGHS B


 3.0 AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVESTOCK OFFICER GRADE II) - Nafasi 39
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kubuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani;
ii. Kuratibu uzalishaji wa mifugokatikamashamba madogo na makubwa ya mifugo;
iii. Kusaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani;

iv. Kuratibuna kuendesha mafunzo ya ufugajibora, usindikaji wa mazao ya mifugo
kwa wataalam wa mifugo na wafugaji;
v. Kufanyamapitio na marekebisho ya miundombinu ya masoko ya mifugo wilayani
kwake na mkoani;
vi. Kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani;
vii. Kufanya soroveya ya rasilimali (resource survey) k.m. mifugo, vyakula vya
mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi;
viii. Kuendesha mafunzokwa mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama
katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo;
ix. Kutafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali;
x. Kufanya tathmini juu ya uharibifu wa mazingira unaotokana na ufugaji katika
wilaya;
xi. Kushiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu
wa malisho;
xii. Kufuatilia,kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo;
xiii. Kuandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo;
xiv. Kufanya kazi nyingine zinazohusianana fani yake kama atakavyoelekezwa na
mkuu wake wa kazi.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyama (Animal Science) au Sayansi ya
Kilimo waliobobea katika Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine au sifa inayolingana na hiyo kutoka chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
3.3 NGAZI YA MSHAHARA
 TGS D


4.0 TABIBU WA KINYWA NA MENO DARAJA LA II (DENTAL THERAPIST GRADE II)
Nafasi 17
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi.
ii. Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida.

iii. Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji
mdogo.
iv. Kushiriki katika kupanga na kutekeleza Huduma za Afya Msingi.
v. Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za Afya za
Mfuko wa Afya ya Jamii.
vi. Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma.
vii. Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji.
viii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada ya Tabibu wa Meno (Diploma in Clinical Dentistry) kutoka
Chuo kinachotambuliwa na Serikali, pia awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari.
4.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGHS B


5.0 MTEKNOLOJIA MAABARA DARAJA II (HEALTH LABORATORY TECHNOLOGIST
GRADE II) - Nafasi 25
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupima sampuli zinazoletwa maabara.
ii. Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa Maabara za
ngazi za juu.
iii. Kufanya kazi za ukaguzi wa maabara, vitendanishi, vifaa, kemikali na hifadhi ya
kemikali.
iv. Kuweka kumbukumbu za maabara ambazo zimepatikana wakati wa uchunguzi.
v. Kufundisha watumishi walio chini yake.
vi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara za afya kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali, ambao wamesajiliwa na Baraza la Waatalam wa Maabara.

5.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGHS B


6.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (OFFICE MANAGEMENT
SECRETARY GRADE II) - Nafasi 74
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;
ii. Kupokea wageni na kuwasikiza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza
kusaidiwa;
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu
wake na ratiba za kazi zingine;
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya
kazi;
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu
husika;
vi. Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali;
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
ix. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) wenye
Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili (Secretarial Studies). Aidha, wawe wamefaulu somo
la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100(100.w.p.m) kwa dakika moja na
kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint,
Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
6.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS C

7.0 MWALIMU DARAJA LA III C - SOMO LA FIZIKIA (PHYSICS SUBJECT) - Nafasi 55
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa
Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
iii. Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya
Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na
unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule;
viii. Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya
Shule.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu
(Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Fizikia au Shahada isiyo ya Ualimu
/Elimu yenye somo la kufundishia la Fizikia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu
(Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na
Serikali.
7.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGTS- D


8.0 MWALIMU DARAJA LA III C - SOMO LA HISABATI (MATHEMATICS SUBJECT)
Nafasi 67
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango
waKazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;

iii. Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya
Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na
unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule; na
viii. Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu
(Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Hisabati AU Shahada isiyo ya
Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Hisabati pamoja na Stashahada ya Uzamili ya
Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika
na Serikali.
8.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGTS D


9.0 MWALIMU DARAJA LA III B - SOMO LA FIZIKIA (PHYSICS SUBJECT) - Nafasi 43
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango
wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
iii. Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya
Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha
na unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
viii. Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya
Shule.

9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu
masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya
Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Fizikia kutoka Vyuo vya Ualimu
vinavyotambulika na Serikali.
9.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGTS C


10.0 MWALIMU DARAJA LA III B - SOMO LA HISABATI (MATHEMATICS SUBJECT)
Nafasi 48
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa
Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
iii. Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya
Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na
unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
viii. Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo
mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya
miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Hisabati kutoka Vyuo vya Ualimu
vinavyotambulika na Serikali.
10.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGTS-C

11.0 AFISA MISITU MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT FOREST OFFICER GRADE
II) - Nafasi 28
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusimamia ukusanyaji mbegu na bustani za miti.
ii. Kukusanya takwimu za misitu.
iii. Kusimamia kazi za upandaji, utunzaji na uvunaji wa miti/misitu. iv.
Kukusanya maduhuli.
v. Kupima mazao ya misitu.
vi. Kufanya doria.vii. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoagizwa na
Msimamizi wake;
11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada katika mojawapo ya fani zifuatazo; Forestry, Agroforestry,
Forest Resources Assessment and Management, Forest Biology, Forest Economics,
Forest Engineering au fani nyingine inayoendana na hiyo kutoka katika Taasisi au Vyuo
vinavyotambulika na Serikali.
11.3 NGAZI YA MSHAHARA
 TGS C


12.0 AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT
ENVIRONMENTAL HEALTH OFFICER GRADE II) - Nafasi 26
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kudhibiti na kuzuia milipuko ya magonjwa;
ii. Kupambana na kuzuia wadudu na wanyama wanaoeneza
magonjwa;
iii. Kusimamia uzikaji wa maiti zisizotambuliwa na zile zinazotokana na magonjwa
yakuambukiza;
iv. Kuandaa taarifa mbali mbali za Afya ya Mazingira katika ngazi ya kata na
kuziwasilisha katika mamlaka husika;

v. Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira, katika kata na kutoa
mrejesho ili kuchukua hatua zinazostahili;Kutoa elimu ya afya ya mazingira kwa
jamii;
vi. Kukagua mazingira katika sehemu zinapotengenezwa vyakula ili kuhakikisha
usalama na afya ya jamii;
vii. Kusimamia sheria za afya ya mazingira katika ngazi ya Kata pamoja na
kusaidiajamii katika kutengeneza sheria ndogondogo;
viii. Kuhamasisha jamii katika kuboresha vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira;
ix. Kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa Huduma za Afya ya Msingi katika ngazi
ya Kata; na
x. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake.
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira kutoka chuo
kinachotambuliwa na Serikali na wawe amesajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya
Mazingira.
12.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGHS B


13.0 MWALIMU DARAJA LA III C - SOMO LA FASIHI YA KIINGEREZA (ENGLISH
LITERATURE SUBJECT) - Nafasi 13
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa
Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
iii. iKufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya
Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na
unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;

vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule; na
viii. Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu
(Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Fasihi ya Kiingereza AU Shahada
isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Fasihi ya Kiingereza pamoja na
Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya
Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
13.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGTS D


MASHARTI YA JUMLA
1. Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi
umri wa miaka 45.
2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
3. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria / Wakili.
4. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
5. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika:Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
6. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa

kada zinazohitaji ‘GPA’ waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi
wa ‘GPA’ kutoka TCU.
8. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
9. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
10. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 17 Septemba, 2026.
11. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti
vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;


KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
 MTAA WA MAHAKAMA,
TAMBUKARELI,
S. L. P. 2320,
DODOMA.


12. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
13. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
14. Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa
kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unazingatia
misingi ya haki, usawa, na uwazi, kwa kuzingatia sifa stahiki zilizoainishwa katika
tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara inayohusika.
Limetolewa na:
KATIBU SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Search Blog
Avatar
Written by System Administrator
ADMIN AUTHOR

Official recruitment manager and platform editor publishing career advices.

Job Details Link

Review full vacancy requirements, salary parameters, and responsibilities for this post.

View Active Listings